Akizungumza na East Africa Radio, Afisa habari wa Baraza la michezo nchini BMT, Najaha Bakari amesema, maandalizi ya uchaguzi huo yamekamilika na wagombea wote pamoja na wapiga kura wapo tayari kwa ajili ya uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Februari 14 mwaka huu uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es salaam.
Najaha amesema, baada ya kumalizika kwa usaili, wenye pingamizi watatakiwa kuwasilisha pingamizi hizo Februari 11 ambapo matokeo ya pingamizi yanatarajiwa kutangaza Februari 12 na baada ya hapo kampeni itaanza siku hiyohiyo baada ya kutoka matokeo ya pingamizi na kumalizika Februari 13 huku uchaguzi ukifanyika kama ulivyopangwa Februari 14.
Najaha amesema, wanatarajia kupata viongozi wanaowahitaji kama wapiga kura watajitokeza wote na kutenda haki katika uchaguzi huo.