Jumanne , 24th Dec , 2024

Klabu ya Simba inaongoza ligi kuu Tanzania bara imekuwa na mwanzo kutokana na kuongoza katika maeneo makuu muhimu kitwakimu.Timu hiyo inaongoza kwenye ufungaji wa magoli ambapo mpaka sasa lihgi kuu imefunga magoli 25 huku ikiwa imeruhusu magoli 5 tu.

Ubora huu wa timu hiyo inayonolewa na Kocha Fadlu Davies unatokana na upana wa kikosio hiko na ubora wa Mchezaji mmojammoja ulioongezeka kwenye kikosi hiko.

Dirisha kubwa la usajili Simba SC iliongeza Wachezaji kila idara ambayo ilikuwa na mapungufu misimu iliyopita.Golini ameongezeka Moussa Camara nyota wa kimataifa kutokea Guinea eneo la beki wa pembeni wameongezeka Kelvin Kijiri na Valentin Nouma ambao wameongeza changamoto ya kiushindani kwa Mohamed Hussein Zimbwe JR na upande wa Shomari Kapombe.

Eneo la beki wa kati ameongezeka Abdulrazack Mohamed Hamza ubora wake umeleta utofauti mkubwa katika sehemu ya beki wa kati.

Sehemu ya katikati ya Uwanja maingizo yaliyofanyika dirisha kubwa la usajili limeleta mabadiliko makubwa kutokana na ubora wa Wachezaji walioingia klabu ya Simba ukilinganisha na misimu mitatu iliyopita,Debora Fernandes Mavambo,Augustine Okajepha na Yusuph Kagoma wameongeza ugumu,ubunifu na ubora ambao umempa kiburi Mwalimu Fadlu kuweza kupumzisha Wachezaji wake na bado kila atakayeingia kikosini anacheza kwa ubora uleule.

Leonel Ateba pamoja Stevin Dese Mukwala,Elie Mpanzu,Edwin Balua pamoja na Radack Chasambi wameongeza magoli sehemu ya ushambuliaji ukilinganisha na safu ya ushambuliaji kikosi hiko katika misimu iliyopita.Upana huu wa kikosi unamfanya Kocha kutokutegemea mchezaji mmoja bali atakayekuwa kwenye kiwango bora atacheza bila kupunguza ubora wa timu hiyo.

Pongezi ziende kwa uongozi wa kikosi cha Simba SC kwa kubaini makosa waliyoyafanya misimu mitatu mfululizo katika idara yao ya usajili wamejirekebisha wameweza kufanya sajili ambazo zimerudisha furaha na imani kwa Mashabiki na Wanachama wa timu hiyo juu ya kushinda ubingwa ligi kuu Tanzania ambao imeukosa kwa misimu mitatu mtawalia sambamba na matamanio ya timu hiyo kutaka kucheza nusu fainali au fainali ya kombe la shirikisho Afrika.