
(kocha wa LIverpool Jurgen Klopp - kushoto.Na kocha wa Man.Utd Ralf Rangnick- kulia)
Kuelekea mchezo huo kocha wa Manchester United Ralf Rangnick amethibitisha kuwa ataendelea kuwakosa nyota wake watano ambao ni mshambuliaji Edinson Cavani, Mlinzi wa kati Raphael Varane,Kiungo Scott MacTominay, mlinzi wa pembeni Luke Shaw na pamoja na kiungo wa ki-brazil Fred ambao bado wauguza majeraha.
Klabu ya Liverpool haijapoteza mchezo kwenye michezo 6 ya mwisho kwenye ligi wakiwa wameshinda michezo 5 na wametoka sare mchezo mmoja. Na katika idadi hiyo ya Michezo 6 ya mwisho kwenye Ligi Mancheater United imeshinda michezo 2 wakitoka sare 2 na wamefungwa 2.
Timu zote zinahitaji ushindi katika mchezo huu, Liverpool wakihitaji ushindi ili kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi katika mbio za ubingwa wampiku Manchester City, Liverpool wana alama 73 katika nafasi ya pili na vinara Manchester City wakiwa na alama 74. na kama Liverpool watashinda mchezo huu basi wataongoza Ligi.
Mashetani wekundu wao wapo kwenye mbio za kuwania nafasi ya 4 kwenye msimamo ili kuweza kushiriki ligi ya Mabingwa ulaya msimu ujao. na kama watapata ushindi kati mchezo huu utawafanya Mancheater United wafikishe alama 57 sawa na Tottenham walioko katika nafasi ya 4 hivi sasa.
Naye nyota wa United Cristiano Ronaldo pia kuna uwezekano wa kutokuwepo katikamchezo wa leo baada usiku wa jana kutangaza kufiwa na mtoto wake mmoja wa kiume kati ya mapacha aliojifungua mchumba wake Georgina usiku wa jana, ila mtoto wa pili ambaye ni wakike amezaliwa salama.
Manchester hawajafurahia taarifa za mabadiliyko ya ratiba ambapo sasa mechi yao dhidi ya Chelsea imesogezwa karibu hadi Aprili 28, badala ya Mei 15 iliyopangwa awali, na hii ina maanisha kwamba sasa lazima United wakabiliane na Liverpool, Arsenal na chelsea kataika michezo iliyofata ndani ya siku 10 zijazo.