Jumatatu , 16th Mei , 2016

Kiungo wa Kimataifa wa Rwanda Haruna Niyonzima amesema baada ya kubeba ubingwa wa Ligi ya Vodacom kazi kubwa iliyopo mbele yao ni fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF).

Kiungo wa Kimataifa wa Rwanda Haruna Niyonzima.

Niyonzima amesema ubingwa umewapa morali wa kufanya vizuri kwenye mechi hizo zinazo wakabili hivyo watapambana kuhakikisha wanafikia malengo waliyojiwekea.

"Tunakwenda Angola tukijua fika kazi iliyopo mbele yetu lakini naamini ubingwa tuliopata wa Ligi Kuu Tanzania Bara umetuongezea ari ya kupambana kwa ajili ya kupata ushindi,"amesema Niyonzoma.

Kiungo huyo amesema mbali na mchezo huo wa Jumanne pia wanamchezo mgumu wa fainali wa Kombe la FA dhidi ya Azam FC nao angependa kushinda ili kuweka historia kwa timu za Tanzania kubeba makombe mawili kwa msimu mmoja.

Niyonzima ndio nahodha msaidizi kwenye kikosi cha Yanga ambacho msimu huu kimeweza kutetea ubingwa wake wa Kigi ya Kuu ya Tanzania Bara msimu huu.