Alhamisi , 4th Feb , 2016

Bondia wa Uingereza Tyson Furry amekataa pambano lake la marudiano na Wladimir Klitschko kufanyika ndani ya meli na kutazamwa na watu 120 tu matajiri.

Furry amesema anataka pambano hilo kutazamwa na watu wengi duniani,na si masharti ya ofa hiyo,inayotaka kusiwe na matangazo ya Televisheni kurusha mpambano huo ukiwa ndani ya meli.

Bingwa huyo wa mikanda ya WBA, WBO na IBO ya uzito wa juu,amesema bado hakuna makubaliano ya wapi atapigana na Klitschko pambano la marudiano,lakini inawezekana ikawa Mashariki ya Kati katikati ya mwaka huu.

Furry mzaliwa wa mji wa Manchester nchini Uingereza alimpiga Klitschko wa Ukrain kwa pointi mwezi Novemba mwaka jana mjini Dusseldorf Ujerumani,na kutwaa mikanda ya WBA,WBO,IBF.