Alhamisi , 15th Oct , 2015

Mwenyekiti wa chama cha NLD Dkt Emmanuel Makaidi ambaye pia alikuwa mgombea ubunge jimbo la Masasi na mwenyekiti mwenza wa UKAWA, amefariki dunia mchana wa leo mkoani Mtwara kwa shinikizo la damu.

Mke wa Mzee Makaidi Mama Modesta Makaidi amethibitisha kutokea kwa kifo hicho, ambapo amesema kuwa Makaidi amefariki leo majira ya saa 6 mchana katika hospitali ya mwambao iliyoko Wilayani Masasi mkoani Mtwara.

"Juzi tukiwa katika harakati za kampeni, alidai anajiskia vibaya, tukampeleka Zahanati, wakamcheki presha wakasema presha imepanda, lakini alipata matibabu akawa na unafuu, lakini leo asubuhi hali ikawa mbaya ndipo tukampeleka Mwambao Hospital, lakini ilipofika majira kati ya saa 5 na saa 6 akafariki" alisema mama Modesta.

Kuhusu taratibu za mazishi Mke wa marehemu Modesta Makaidi amesema kuwa taarifa zitatolewa baadaye lakini kuna uwezekano mkubwa wa mwili wake kupelekwa jijini Dar es salaam.