Katika taarifa yake, Katibu wa TWA Gola Kapipi amesema, lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha mchezo huo unarudi katika hadhi yake ya zamani kwa kuanza na mashindano mbalimbali katika shule za msingi.
Kapipi amesema, mikakati yao inatarajia kuanza mwezi ujao katika shule mbalimbali za jijini Dar es salaam kabla ya kuamia mikoani ambapo wanaamini watapata sapoti kutoka kwa wadau wa mchezo huo.


