Jumanne , 25th Aug , 2015

Chama cha mpira wa Wavu TAVA kimesema kimejipanga vizuri ili kuweza kuepuka lawama kuhusiana na waamuzi watakaochezesha mashindano ya Wavu Klabu Bingwa Taifa yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi hapo kesho jijini Arusha.

Akizungumza na East Africa Radio, Makamu mwenyekiti wa TAVA Muharame Mchume amesemamiaka iliyopita waliokuwa waamuzi waliokuwa wakiichezesha michuano hiyo walikuwa ni wachezaji suala ambalo lilikuwa likileta lawama kwa baadhi ya timu kuona mchezo hauchezwi kwa haki.

Mchume amesema, wamechukua waamuzi ambao wanamafunzo na watakuwa tofauti na miaka iliyopitita wakiwa wamepata elimu ili kuweza kuchezesha michuano hiyo kwa haki na usawa.