Alhamisi , 29th Feb , 2024

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imesema haitarajii kufanya mabadiliko ya ratiba kutokana na ushiriki wa timu za Simba SC na Yanga SC kwenye michezo ya Ligi ya mabingwa barani Afrika iwapo timu zote hizo mbili zitafuzu kuelekea hatua za mbele zaidi kwa pamoja.

Afisa habari wa Bodi ya ligi  Karim Boimanda amesema kuwa   ratiba waliyoipanga kwa sasa inawapa nafasi Simba   na Yanga  kushiriki mashindano hayo mpaka mwisho na kusisitiza hakutakuwa na mabadiliko yoyote kutokana na ushiriki wao ndani ya michezo hiyo

" Tutarajie ratiba ikitekelezwa vizuri bila kuwa na michezo ya viporo   malengo yetu ni kuona Ligi inamalizika kwa wakati na hatutarajii kuwa na viporo vingi, amesema  Boimanda.

Katika hatua nyingine,Boimanda amezitaka  Klabu zote kufuata kanuni na sheria za Ligi kwani wakifanya hivyo wataiboresha zaidi Ligi Kuu ya Tanzania Bara ambayo kwa sasa inashika nafasi ya 6 kwa ubora barani Afrika .