Ijumaa , 7th Nov , 2014

Kocha wa Timu ya Taifa ya Judo, Zaid Khamis amesema anatarajia kutumia mashindano ya Judo Taifa yanayotarajiwa kuanza hapo kesho jijini Dar es saalaam, kuweza kupata vijana watakaounda kambi ya muda mrefu ya Timu ya taifa.

Akizungumza na East Africa Radio, Zaid amesema mshindi wa kwanza mpaka wa tatu wataingia kambini lakini atachagua vijana ambao anaamini watakuwa na uwezo kwa ajili ya kuendelea na mazoezi kwa ajili ya mashindano ya Kanda ya Tano yatakayofanyika hapo mwakani huku Tanzania ikiwa nchi mwenyeji.

Zaid amesema, wameamua kuwa na kambi ya timu ya taifa ya muda mrefu ili kuweza kuwapa vijana watakaoingia kambini mbinu mbalimbali za mchezo wa Judo zitakazowasaidia kuweza kufanya vizuri katika mashindano mengine ambayo yatajitokeza.