Jumanne , 10th Feb , 2015

Viongozi wa vyama vya soka vya mikoa, Viongozi wa timu na wachezaji wanaoshiriki katika michuano ya Ligi Daraja la kwanza zimetakiwa kucheza michezo yao kwa kufuata sheria 17 za soka hapa nchini.

Akizungumza na East Africa Radio, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF, Baraka Kizuguto amesema, sheria hizo zinatakiwa kuwaongoza katika mechi hizo, hivyo wanatakiwa kuwa makini kwa kufuata sheria hizo ili kuanza na kumaliza salama mchezo.

Kizuguto amesema, atakayebainika kukutwa na hatia yoyote Shirikisho halitapindisha sheria kwa ajili ya kumnusuru mtu na wanaamini kwa kufuata Sheria hizo mechi zitachezwa kwa kuzingatia haki kwa kila timu.