Jumatano , 24th Nov , 2021

Manchester United na Chelsea zimefuzu hatua ya 16 bora, Ligi ya mabingwa barani ulaya baada ya kushinda michezo ya raundi ya tano ya hatua ya makundi jana usiku. Chelsea imeifunga Juventus mabao 4-0 na Manchester United imeinyuka Villarreal mabao 2-0.

Wachezaji wa Chelsea wakishangilia moja ya goli kwenye ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Liverpool

Chelsea walikuwa katika uwanja wao wa nyumbani Stanford Bridge na mabao ya ushindi katika mchezo huo wa kundi H yamefungwa na Trevoh Chalobah, Callum Hudson-Odoi, Reece James na Timo Werner. Kwa matokeo hayo The blues inafikisha alama 12 sawa na Juventus tofauti ikiwa ni magoli ya kufunga na kufungwa na timu zote zimefuzu hatua ya 16, mchezo mwingine wa kundi hilo Malmo dhidi ya Zenit ST. petrsburg ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.

The Red Devils Manchester United wamekata tiketi ya kufuzu hatua ya 16 bora baada ya kufikisha alama 10 katika msimamo wa kundi F. Katika ushindi huo wa mabao 2-0 mabo ya Manchester united yamefungwa na Cristiano Ronaldo aliyefunga bao lake la 6 kwenye michuano hii msimu huu na akifunga katika mchezo wa 5 mfululizo lakini pia amefikisha mabao 800 kwenye maisha yake ya soka, Jadon Sancho alifunga bao la pili na ni goli lake la kwanza tangu ajiunge na klabu hiyo. 

Mchezo mwingine wa Kundi F Atalanta walitoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya Young Boys, katika msimamo wa kundi hilo Manchester United wana alama 10 wameshafuzu, Villarreal nafasi ya pili alama 7, Atalanta nafasi ya 3 alama 6 na Yanga Boys wana alama 4.

Mpaka sasa ni timu sita (6) zilizofuzu hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa barani ulaya baada ya michezo ya raundi ya 5 ya hatua ya makundi Chelsea na Manchester United wanaungana na Liverpool, Ajax, Juventus na Bayern Munich.