Hamis Dambaya (Aliyesimama) alipokuwa mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba
Katika salamu hizo, TFF imempa pole Dambaya kwa msibu huo mzito uliomfika na kusema kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini, Shirikisho liko pamoja nao katika kipindi hichi kigumu cha maombelzo ya misiba hiyo.
Mkewe Hamis Dambaya, mwanaye na mama mkwe wake wamefariki katika ajali ya basi la Simba Mtoto iliyotokea leo asubuhi katikati ya eneo na Muheza na Hale wakati wakiwa safarini kuelekea jijini Dar es salaam wakitokea mkoani Tanga.
Katika ajali hiyo, watu 11 wamepoteza maisha wakiwemo madereva wawili wa magari yaliyogongana na 29 kujeruhiwa.





