
Langa Lesse Bercy
Timu ya Congo inadaiwa kukiuka kanuni za mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 kwa kumchezesha mchezaji huyo licha ya kutokuwa na umri stahiki.
Afisa Habari wa TFF Alfred Lucas amesema Congo inafanya ujanja wa kutompeleka mchezaji huyo kwenye vipimo ili kuepuka adhabu ya kufungiwa kwa miaka mitatu.
Langa Lesse Bercy, alichezeshwa kwenye mechi ya timu ya vijana ya Congo dhidi ya Serengeti Boys ya Tanzania katika Mashindano ya kufuzu Fainali za Afrika chini ya miaka 17, mwezi Oktoba jijini Brazzaville, na Congo kuitoa Tanzania kwa jumla ya sare 3-3, lakini Congo ikafuzu kwa bao la ugenini.
TFF ilikata rufaa na kutaka mchezaji wa Congo afanyiwe vipimo vya umri, lakini mchezaji huyo, hakufika Cairo, Novemba 17, kwa madai kuwa yupo eneo ambalo si salama, huko Congo.