
kikosi cha timu ya Green Warriors kwenye picha ya pamoja kabla ya moja ya mechi ya ligi daraja la pili msimu huu.
Akizungumza na East Africa Radio mkuu wa ufundi klabuni hapo Juma Mbwana amesema wamekuwa wakishangazwa na maamuzi ya marefa yasiyo na haki hali inayopelekea kuzipa nafasi timu zisizo na uwezo kusonga mbele kwenye mashindano.
Katika hatua nyingine mkurugenzi huyo amesema licha ya kuongoza kundi A ligi daraja la pili kwa pointi zao saba wamepania kushinda mechi zao mbili za hivi karibuni dhidi ya Transit Camp na Abajalo kabla ya kuishukia Mji Njombe katika raundi ya pili ya kombe la FA disemba 24 mwaka huu.
Naye msemaji wa timu hiyo Wille Elius amewaatahadharisha wapinzani wao kukaa chonjo kwa kuwa usajili waliofanya msimu huu ni imara ambao wanauhakika kila timu watakayokutana nayo itaambulia kipigo cha aina yake.