TFF
Kauli hiyo aliitoa baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu Tanzania bara, ambapo Yanga ilicheza ana Lipuli FC na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika Uwanja wa CCM Samora mjini Iringa.
Katika taarifa rasmi iliyotolewa na Yanga hii leo kupitia kwa Kaimu Katibu Mkuu, Simon Patrick, pamoja na kumfuta kazi kocha huyo pia klabu itahakikisha anaondoka nchini haraka iwezekanavyo.
"Kutokana na kauli zisizo za kiungwana na kiuanamichezo. Uongozi wa Yanga umeamua kumfuta kazi kocha Luc Eymael kuanzia leo Julai 27, 2020 na kuhakikisha anaondoka nchini haraka iwezekanavyo", imesema taarifa ya Yanga.
Pia Shirikisho la Soka Tanzania TFF limetoa taarifa yake kufuatia tukio hilo ambapo limesema kuwa litamfikisha katika vyombo husika kocha kutokana na matamshi yake ya kibaguzi kwa mashabiki wa timu hiyo. Pia litamripoti kwa Shirikisho la Soka Duniani FIFA.






