Jumatatu , 10th Mei , 2021

Bodi ya ligi nchini TPLB imesema suala la mechi ya watani wa jadi kuahirishwa litajadiliwa leo Mei 10, 2021, kwenye Kamati ya Saa 72. 

Mashabiki wa Simba SC na Yanga SC

Bodi pia imesema ilipokea maelekezo ya kubadili muda wa mechi kutoka Shirikisho la Soka Nchini (TFF) Saa 7:00 mchana, ndipo ikavijulisha vilabu kuwa mechi itapigwa saa 1:00 usiku badala ya saa 11:00 jioni.

Mapema jana TFF ilitoa taarifa ikiitaka Bodi ya ligi kueleza kwanini mchezo uliahirishwa lakini Bodi nayo imesema ilipokea maelekezo kutoka TFF.

Soma taarifa kamili ya TPLB