Alhamisi , 6th Mar , 2014

Timu ya Taifa ya soka ya wanawake ya Tanzania kushiriki mashindano mengi kimataifa

Shirikisho la soka nchini TFF limesema kuwa kutokana na uchache wa mashindano ya wanawake barani Afrika kuanzia sasa watakua wakiiingiza timu ya wanawake Twiga Stars katika kila shindano litakalokua mbele yao.

Afisa Habari wa TFF Boniface Wambura amesema kuwa mara baada ya timu hiyo kutolewa na timu ya taifa ya wanawake ya Zambia Shepolopolo katika michuano ya kusaka tiketi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika, hivi sasa wameiingiza timu hiyo katika michuano ya All Africa Games itakayofanyika Congo Brazaville hapo mwakani.

Wambura amesema kuwa wanachosubiri hivi sasa ni ratiba ya michuano hiyo ndipo waanze maandalizi ya michuano hiyo.