Kikosi cha Simba na makocha wake
Klabu hiyo kupitia kwa kampuni yake ya Simba Sports Club Limited, imeelezwa kumteua Patrick Rweyemamu ambaye ni mwanachama wa muda mrefu wa Simba.
Rweyemamu amekuwa kocha wa muda mrefu wa kikosi cha vijana cha Simba na hatosahaulika kutokana na mchango wake mkubwa katika kuwalea wachezaji kama Jonas Mkude, Ndemla, Manyika Jr na wengine.
Mbobezi huyo wa soka la vijana alikuwa kocha wa timu ya vijana ya Simba wakati ambao kocha mkuu alikuwa ni Patrick Phiri ambaye mara nyingi alishirikiana naye kuwapandisha vijana kwenye timu kubwa.
Patrick Rweyemamu
Rweyemamu mbali na kushika nafasi tofauti za uongozi ndani ya klabu ya Simba, aliwahi pia kuwa mjumbe wa kamati mbalimbali ndani ya Shirikisho la SokaTanzania (TFF) hasa zile zinazohusu soka la vijana.
Nafasi ya meneja ndani ya klabu ya Simba inashikiliwa na mchezaji wa zamani Mussa Mgosi ambaye pia ni kocha msaidizi wa timu ya vijana ya Simba chini ya miaka 20.