Alhamisi , 28th Jul , 2016

Rais wa shirikisho la Mpira wa kikapu nchini TBF Mhandisi John Bandiye anatarajiwa kufungua mafunzo ya waamuzi wa mchezo huo yatakayofanyika hapo kesho viwanja wa kukuza michezo vya JK Park jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi wa masuala ya ufundi wa TBF Manase Zabron amesema, mafunzo hayo yanatarajiwa kushirikisha waamuzi 30 kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.

Zabron amesema, waamuzi wote waliopo jijini Dar es salaam na mikoa ya jirani wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mafunzo hayo muhimu na yenye lengo la kukuza na kuuendeleza mchezo huo hapa nchini.