Jumanne , 26th Aug , 2014

Vipaji na kujituma kunakooneshwa na wachezaji wa michezo mbalimbali kutoka Tanzania katika michuano ya shule za sekondari kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki kunawapa matumaini ya kufanya vema katika michuano hiyo msimu huu.

Baadhi ya wachezaji wa timu za shule za sekondari za EA wakichuana katika mechi ya michuano ya FEASSA.

Timu za sekondari za Tanzania zimeendelea kung’ara katika michuano ya timu za shule za sekondari kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki FEASSA inayoendelea katika viwanja mbalimbali jijini Dar es salaam

Ambapo muhtasari wa michezo umeshuhudia timu ya soka ya wanawake ya Makongo sekondari ikiichabanga bila huruma timu ya wanawake ya sekondari ya wasichana ya Butere toka Kenya kwa mabao 4-1 katika mchezo ambao watanzania hao walionekana kucheza kwa kasi na umakini mkubwa kiasi cha kuwadhibiti wapinzani hao toka Kenya.

Na mara baada ya mchezo huo tumezungumza na kocha wa timu ya Makongo sekondari Milambo Milambo ambaye amesema ushindi huo ni mwanzo wa kasi yao kuelekea hatua za juu zaidi

Naye nahodha wa timu hiyo ya Makongo Shelda Boniface amesema wamefurahia ushindi huo mkubwa ambao hawakuutegemea kutokana na wapinzani wao kuonekana na maumbo makubwa ukilinganisha na wao na hivyo kuwafanya kupatia wakati mgumu katika kuwakabiri wapinzani wao lakini wanashukuru kwa kuwa wameweza kukabiliana na upinzani huo na hatimaye kuibuka na ushindi huo mkubwa.