Jumatatu , 14th Dec , 2015

Watani wa jadi, Coastal Union 'Wagosi wa Kaya' na Afrika Sports 'Wana Kimanumanu' wamemaliza Tanga derby kwa kutoshana nguvu baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, hapo jana.

Juma Mahadhi ndiye aliyefunga bao la Coastal Union huku Mohammed Mtindi naye akiwafungia Wana Kimanumanu bao lao.

Wakati huo huo, JKT Ruvu wamewapa somo la “kijeshi” maafande wa Tanzania Prisons kwa kuwachapa mabao 4-1 katika muendelezo wa michuano ya Ligi kuu.

Mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, Samwel Kamuntu alifunga bao moja, Mussa Juma akatupia moja na Michael Aidan akifunga mawili huku lile la Prisons likifungwa na Mohammed Mkopi.