Ijumaa , 30th Mei , 2014

Shirikisho la soka nchini limesema kuwa kikosi cha taifa Stars kimewasili nchini Zimbabwe na kiko tayari kuwavaa wazimbabwe hapo kesho kutwa mjini Harare.

kikosi cha taifa stars kikiwa safarini nje ya nchi.

Msafara wa watu 30 wa Taifa Stars unaojumuisha wachezaji, benchi la ufundi na viongozi umewasili nchini Zimbabwe salama tayari kwa mechi ya marudiano ya kusaka tiketi ya kucheza fainali za Afrika hapo mwakani nchini Morocco

Afisa habari wa TFF Boniface Wambura ameiambia Eatv kuwa taifa stars iko tayari kwa mechi hiyo ambayo itachezwa Juni Mosi mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Harare, ambapo pia Taifa Stars inataraji kuongezwa nguvu kutokana na ujio wa nyota wawili wanaokipiga katika klabu ya TP Mazembe ya Congo DRC

Aidha Wambura amesema ujio wa wanandinga hao utampa wigo mpana kocha mkuu Mart Nooij kuweza kuwa na washambuliaji wa kutosha hasa ikizingatiwa uwepo wa wachezaji hao ni chachu ya ushindi na hilo lilijidhihirisha katika mchezo wa kwanza ambao stars ilishinda bao 1-0 kwa goli safi la mshambuliaji John Bocco akipokea basi safi kutoka kwa Thomas Ulimwengu ambaye kabla yakutoa pasi hiyo aligongeana paso kadhaa na Mbwana Samata.