“Kuna changamoto kidogo ya usafiri. Hatukufanikiwa kupata tiketi za timu nzima kwa mara moja kwahiyo walioanza kuwasili nchini jana ni wachezaji na viongozi 15.”
“Kuna baadhi yao watafika leo wengine kesho. Pia kuna wachezaji ambao wamerejea moja kwa moja kwenye nchi ambako timu zao wanazochezea” Katibu Gerson Msigwa.
Taifa Stars ilitupwa nje ya Fainali za kombe la Mataifa Afrika na kuondoka na alama 2 katika kundi F ambazo zilikuwa na timu ya Morrocco,Zambia ,DRC na Tanzania