Jumatano , 24th Jun , 2015

Kikosi cha wachezaji 16 cha Timu ya Taifa ya mpira wa Netiboli inatarajiwa kuondoka kesho kuelekea nchini Botswana kujiandaa na mashindano ya Afrika yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia Juni 27 mwaka huu kwa kushirikisha nchi takribani 19

Akizungumza jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli nchini CHANETA, Anna Kibira amesema, kikosi kimejiandaa vizuri kwa ajili ya mashindano hayo na ana amini kwa maandalizi waliyoyafanya wachezaji.

Kibira amesema, anaiomba Serikali kuisaidia timu hiyo kwa ajili ya malazi kwani kiasi walichokipata mpaka sasa hakijakidhi majitaji ya timu hiyo ambayo yanaweza kuwasaidia kwa ajili ya kuweza kufanya vizuri zaidi katika mashindano hayo.