Jumatatu , 1st Jun , 2015

Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars imeingia kambini leo kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON).

Katika taarifa yake, Afisa habari wa Shirikisho la soka nchini TFF, Baraka Kizuguto amesema, kikosi kilichoingia kambini kinawajumuisha wachezaji waliocheza michuano ya Cosafa nchini Afrika Kusini mwishoni mwa mwezi Mei, wachezaji 20 walioanza kambi tangu wiki iliyopita na wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nchini Congo DR.

Taifa Stars inatarajiwa kuendelea na mazoezi kwa muda siku mbili kabla ya siku ya alhamis kusafiiri kuelekea Addis Ababa nchini Ethiopia ambapo itaweka kambi ya wiki moja kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri.

Wachezaji walioingia kambini leo ni Deogratias Munish, Mwadini Ali, Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Haji Mwinyi, Aggrey Morris, Salum Mbonde, Erasto Nyoni, Saimon Msuva, Hassan Dilunga, Joram Mgeveke, Juma Liuzio, Said Ndemla, Mwinyi Kazimoto, Abdi Banda, John Bocco, Mrisho Ngasa, Salum Abubakar, Ibrahim Hajibu, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta.

Wachezaji waliopo kambini tangu wiki iliyopita ni Nadir Haroub, Juma Abdul, Salum Telela, Peter Manyika jr, Jonas Mkude, Hassan Isihaka, Mohamed Hussein, Aishi Manula, Frank Domayo, Mudathir Yahya, Kelvin Friday, Malimi Busungu, Bennedict Tinoco, Rashid Mandawa, Atupele Green, Haroun Chanongo, Emmanuel Simwanda, Said Mohamed, Andrew Vicent, Gadiel Michael, Deus Kaseke.

Mechi kati ya Misri dhidi ya Tanzania inatarajiwa kuchezwa Juni 14 mwaka huu katika uwanja wa Borg El Arab pembeni kidogo ya jiji la Alexandria.

Wakati huo huo Tanzania imepata mwaliko wa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya Rwanda kati ya Juni 6, 7 mwaka huu jijini Kigali, kwenye kumbukumbu ya mauaji ya kimbali, Tanzania itapeleka kikosi cha vijana U23 katika mchezo huo utakaochezwa mwishoni mwa wiki.

Kufuatia kupata mwaliko huo kikosi cha U23 kitaondoka nchini Juni tano mwaka huu kuelekea nchini Rwanda kikiwa na wachezaji 18 chini ya kocha Salum Mayanga.

Kocha wa Mtibwa Sugar Mecky Maxime ameongezwa kwenye benchi la ufundi litakalokwenda Ethiopia kisha nchini Misri kufuatia kocha Salum Mayanga kuwa na timu ya U23 nchini Rwanda.