Jumatatu , 24th Aug , 2015

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzani Taifa Stars kimeondoka leo kuelekea nchini Uturiki kuweka kambi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria huku kikimuacha mlinda mlango wake Aishi Manula.

Kikosi hicho kinachojiandaa na mechi ya kuwania kufuzu kucheza michuano ya mataifa ya Afrika Septemba 5 mwaka huu kimemuacha mlinda mlango huyo kutokana na kuwa majeruhi.

Katika taarifa yake kocha wa Stars Charles Boniface Mkwasa amesema wachezaji wakulipwa wa Tanzania wote watajiunga na Stars kulingana na kalenda ya FIFA pindi itakapohitaji wachezaji wa vilabu kwenda kuzitumikia timu zao za taifa.