Stars jana ilipoteza mchezo wake wa kwanza kuwani kufuzu fainali za AFCON mwaka 2017 baada ya kufungwa na Misri bao 3-0.
Stars ilicheza vizuri kipindi cha kwanza na hasa sehemu ya ulinzi ilifanya kazi ya ziada kuokoa mashambulizi ya washambuliaji wa timu ya Misri na kupelekea kwenda mapumziko 0-0.
Kipindi cha pili Misri walifanya mabadiliko yaliyowapelekea kupata mabao hayo matatu ndani ya dakika 10.


