Jumatano , 3rd Jun , 2015

Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars inatarajia kuondoka kesho kuelekea nchini Ethiopia kwa ajili ya kujiandaa na mechi dhidi ya timu ya Misri kufuzu michuano ya AFCON.

Katika taarifa yake, Afisa habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF, Baraka Kizuguto amesema, timu hiyo inayoelekea nchini Misri itaondoka na wachezaji wengi ambao baadhi yao hawashiriki mashindano ya CHAN.

Kizuguto amesema, timu hiyo imeongezewa nguvu kwa upande wa benchi la ufundi baada ya kocha msaidizi kubaki na timu itakayoelekea Rwanda hivyo kocha wa Timu ya Mtibwa Mecky Mexime atakuwa kocha msaidizi wa Stars.

Kizuguto amesema, Timu itakaa Ethiopia kwa siku sita baada ya hapo itaelekea nchini Misri huku ikiwa na wachezaji wakimataifa wa Kilipwa ambao ni Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaocheza nchini Kongo ambao wamewasili hapo jana.

Kizuguto amesema, wachezaji 18 watakaoelekea nchini Rwanda kushiriki kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari wataondoka Ijumaa wakiwa chini ya Kocha Msaidizi Salum Mayanga.