
Raphael Varane
6. Ni nafasi iliyomaliza timu ya Polisi Tanzania kwenye msimamo wa Ligi kuu Tanzania bara msimu uliomalizika wa 2020-21, na klabu hiyo hapo jana imetoa ufafanuzi juu ya taarifa zinazogaa mitandaoni kuwa wamemtelekeza mchezaji wao Mathias Mdamu ambaye amelazwa katika Hospital ya taifa ya Muhimbili akiuguza majaraha baada ya kupata ajari akiwa na kikosi hicho.
Msemaji wa Polisi Hassan Juma kupitia Kipenga ya Eastafrica Radio amesema wao kama klabu hawajashindwa kumuudumia Mdamu na bado wanamuhudumia kama mchezaji wao na haya yanayosemwa ni sehemu ya maisha na huku akisistiza wao ndio waliomuhudumia kuanzia akiwa KCMC Moshi na walimsafirisha kuja Dar es salaam kwa Gharama zao, lakini pia ameweka wazi kuwa familia ya mchezaji huyo ndiyo iliyoomba aletwe jijini Dar es salaam kutokea Moshi ili awe karibu na familia, Polisi imebidi watoe ufafanuzi huu baada ya taarifa kuenea kuwa hawamuhudumii mchezaji na ndugu pekee ndio ambao wamekuwa wakimuhudumia pasipo na usaidizi kutoka kwa timu hiyo.
Mathias Mdamu alivunjika miguu yote miwili katika ajali ambayo ilitokea taklibani wiki mbili zilizopita majira ya Asubuhi wakati kikosi hicho kikitoka mazoezini.
5. Idadi ya mabao aliyofunga mshambuliaji wa Simba SC Chris Mugalu mwezi Julai kwenye ligi Kuu soka Tanzania bara na mabao hayo yamemfanya ashinde tuzo ya mchezaji bora wa VPL mwezi Julai akiwashinda wachezaji Charles Ilamfya wa KMC na Juma Luzio wa Mbeya City aliokuwa akishindana nao.
Mwezi Julai Simba ilicheza michezo mitano ilishinda michezo mitatu, sare mchezo mmoja na walifungwa mchezo mmoja ambapo Mugalu alifunga mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya KMC mchezo ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0, akafunga tena mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya Namungo ambao Simba ilishinda mabao 4-0 na alifunga bao 1 kwenye mchezo dhidi ya Coastal ambao Simba walishinda kwa mabao 2-0.
Na kocha wa Yanga Mohamed Nasreddine Nabi ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwezi julai akiwashinda Mathias Lulle wa Mbeya City na Didier Gomes Da Rosa wa Simba.
4. Ni mataji ya Grandslams aliyoshinda mwanadada anayeshikilia nafasi ya pili katika viwango vya ubora Duniani upande wa Wanawake katika mchezo wa Tenisi, Naomi Osaka ameondolewa katika mashindano ya Olimpiki baada ya kufungwa na Marketa Vondrousova raia wa Czech.
Bingwa huyo mara 4 wa Grand slam mwenye umri wa miaka 23, ametupwa nje ya michuano kwa kufungwa kwa seti mbili za 6-1,6-4 dhidi ya Marketa ambaye anashikilia nafasi ya 42 katika viwango vya ubora Duniani kwa Wanawake.
Akizungumzia juu ya kuondolewa kwake, Osaka amesema sababu ya yeye kupoteza inawezekana ni kutokana na ushiriki wake kwa mara ya kwanza katika mashindano hayo ya Olimpiki. Osaka ambaye ndiye bingwa wa mashindano ya wazi ya Marekani na yale ya Australia alikuwa akishiriki michuano ya Olympic kwa mara ya kwanza tangu, ambayo yanafanyika katika aridhi ya nyumbani kwao nchini Japan.
3. Ni miaka aliyosaini Milutin ‘Micho’ Sredojevic kuwa kocha wa timu ya taifa ya Uganda Creance, Shirikisho la Soka nchini Uganda limemtangaza mkufunzi huyo raia wa Serbia kuwa kocha mpya na akiwa anarejea kukinoa kikosi hicho kwa mara ya pili baada ya hapo awali kukinoa kikosi hicho kati ya mwaka 2013 hadi 2017 na alikiwezesha kikosi hicho kufuzu fainali za Afcon mwaka 2017 ambapo ilikuwa ni kwa mara ya kwanza Tangu mwaka 1978.
Kibarua kinacho mkabili mbele yake ni kuhakikisha Uganda inafuzu kucheza fainali za kombe la Dunia na katika michezo ya kuwania nafasi hiyo Uganda imepangwa kundi E sambamba na majirani zao Kenya, Rwanda, na timu ya taifa ya Mali. Taarifa iliyotolewa na shirikisho la nchi hiyo FUFA limeweka wazi kuwa mkataba wa kazi wa kocha huyo utaanza Rasmi Agosti 1 na Agost 3 ataongea na wanahabari.
Micho anatajwa kuwa ni miongoni mwa makocha wanaolijua vizuri soka la Afrika mpaka sasa ameshafundisha katika mataifa takliban 8 barani Afeika ikiwemo Tanzania ambapo alikinoa kikosi cha Yanga mwaka 2007.
2. Ni idadi ya wachezaji waliosajiliwa na klabu ya Manchester United katika dirisha la usajili la majira haya ya kiangazi ambalo bado lipo wazi mpaka August 31, hii ni mara baada ya hapo jana klabu hiyo kudhibitisha kuwa imefikia makubalia na klabu ya Real Madrid ya Hispania ya kumnunua beki wa kati Raphael Varane raia wa Ufaransa kutoka katika kikosi cha mabingwa Kihistoria wa ulaya.
Usajili wa Varane unakuwa wapili kwa Man United baada ya hapo awali kukamilisha usajili wa winga Jadon Sancho kutoka Borussia Dortmund ya Ujerman. Klabu ya Madrid nayo imethibitisha kuondoka kwa mlinzi huyo na imemshukuru kwa utumishi wake. Varane alijiunga na Madrid mwaka 2011 na ameshinda mataji manne (4) ya ligi ya mabingwa Barani ulaya na ubingwa wa Ligi Kuu Hisapnia La liga mara tatu (3) akiwa na Madrid, na sasa kinachosubiliwa ni Varane kufanya makubaliano binafsi na mshetani wekundu na kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kutangazwa rasmi.
1. Ni Medali pekee ya Gold iliyotwaa taifa la Bermuda katika michezo ya Olimpiki na limekuwa taifa la kwanza lenye watu wachache kushinda medali ya dhahabu likuwa na idadi ya watu 63,000. Medali hiyo ya pekee imekwenda katika taifa hilo baada ya Flora Duffy kumaliza wa kwanza kwenye mchezo wa Triathlon ambao hujumuisha michezo mbali mbali ikiwemo kuogelea, kukimbia umbali mrefu, na kuendesha baiskeli.
Bermuda ni visiwa vinavyopatikana kaskazini mwa bahari ya Atlantic, na hapo awali waliweka rekodi yakuwa taifa la kwanza lenye watu wachache kushinda medali kwenye Olympic ilikuwa mwaka 1976 ambapo walishida medali ya Bronze yani Shaba, na sasa wameshinda goldi yao ya kwanza.