
Bondia Hassan Mwakinyo
6. Ni sawa na idadi ya siku zimepita tangu kuvuja kwa sauti ya mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Simba Haji Manara, sauti ambayo ilisikika Haji akimjibu mtendaji mkuu wa klabu hiyo Barbara Gonzalez juu ya tuhuma za kuihujumu klabu ya Simba dhidi ya Yanga
Na msemaji huyo alipanga kuongea na vyombo vya habari hapa jana kutolea ufafanuzi juu ya mambo mbali mbali kuhusu sakata hilo lakini alisitisha mpango huo kwa kuandika kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram akiweka wzi kuwa hatafanya hivyo baada ya kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi na wadau wa klabu hiyo. Sehemu ya ujembe wake ulisomeka,
Sitaongea lolote Kwa sasa nikiamini katika maslahi makubwa ya Simba, team ya maisha yangu.Captain wangu @john_22_bocco always naamini ktk ww Nahodha wa mfano, tuliongea nikiwa ktk bad mood lakini nasaha zako na Kwa heshma ya jana ninakataaje Kwa mfano kukusikiliza? Washabiki wote wa Simba na Waandishi mliokuwa na hamu na press yangu Am Sorry, acheni Ibilisi aepukwe ngoja tusubiri mchanga wa Pwani.
5. Ni idadai ya kadi ambazo zilitolewa kwenye mchezo wa fainali ya kombe la Azam sports federation Cup kati ya Simba dhidi ya Yanga mchezo ambao Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0, na katika kadi hizo 5 nne zilikuwa za njano tatu walionyeshwa wachezaji wa Simba na moja ilikwenda kwa mchezaji wa Yanga na kadi moja ilikuwa ni nyekundu ambayo alionyeshwa kiungo wa Yanga Mukoko Tonombe kipindi cha kwanza na katolewa mchezoni.
Kutoka kwa mukoko kwa kuonyeshwa kadi hiyo nyekundu inatajwa kama moja ya sababu ya Yanga kupoteza mchezo huo, sasa mchezaji huyo amewaomba radhi mashabi na wapenzi wa Yanga kwa kupata kadi hiyo kwenye mchezo huo na huu ndio ulikuwa ujembe wake wa kuomba msamaa ameandika Tonombe
Nachukuwa fursa hii kuomba radhi mashabiki pamoja na viongozi na benchi la ufundi kwa kilicho tokea katika mchezo Wa final wa yanga vs simba. Kwamba sijakusudia kupewa kadi nyekundu ambayo labda ndo ilikuwa sababu yakupoteza mchezo huo. Naipenda sana team yangu yanga DAIMA MBELE NYUMA MWIKO
4. Ni miaka ambayo inatajwa beki Raphael Varane atasaini kuitumikia klabu ya Manchester United akitokea Real Madrid pindi uhamisho wake wa kujiunga na mashetani hao wekendu kutoka jiji la Manchester. Inaripotiwa kuwa Manchester united imefanya makubaliano binafasi na beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa lakini pia inatajwa Real Madrid wamekubali kumuuza Varane kwa ada ya uhamisho ya pauni million 35 ambayo ni Zaidi ya billion 112 kwa pesa za kitanzania.
Usajili wa Varane mwenye umri wa miaka 28 ambaye ni mshindi mara nne wa klabu bingwa Ulaya na mshindi mara tatu wa Ligi Kuu Hisapnia La liga akiwa na Real Madrid, ukikamilika utakuwa usajili wa pili Man United wanaukamilisha katika dirisha hili la majira ya kiangazi baada ya kutangaza usajili wa Jadon Sancho kutoka Borussia Dortmund lakinpia wanahusishwa na mlinzi wa kulia wa kimataifa wa England anaecheza Atletico Madrid Kieran Trippier.
3. Ni nafasi ambayo klabu ya Liverpool ilimaliza msimu uliopita wa 2020-21 ikiwa na alama 66 ikizidiwa alama 17 na mabingwa Manchester City, majeruhi kwa wachezaji muhimu wa kikosi hicho hususani wa safu ya ulinzi Virgil Van Dijik na Joe Gomez ilitajwa kuwa ni sababu iliyowafanya washindwe kutetea ubingwa wa VPL ambao waliutwaa kwa mara ya kwanza baada ya miaka 30 kupita.
Sasa kuelekea msimu ujao wa 2021-22 kocha Klopp amesema hana uhakika juu ya hali ya walinzi wake hao kama watakuwa tayari kucheza michezo ya mwanzoni mwa msimu na katika kuhakikisha hilo, Klopp amesema atampa walau dakika 20 za kucheza Virgil van Dijk kwenye mchezo wa kirafiki kesho Alhamisi dhidi ya Hertha Berlin ilikuangalia utimamu wake umefikia hatua gani na ameweka wazi kuwa Joe Gomez atampa nafasi kwenye mchezo wa Agosti 8 watakao cheza dhidi ya Athletic Bilbao.
2. Ni nafasi alizopanda bondia Hassan Mwakinyo wa Tanznaia kwenye viwango vya ubora wa mabondia barani Afrika kwa mabaondia wa uzito wa Super Welterweight hii ni kwa mujibu wa vingo vipya vya ubora wa mabondia.
Mwakinyo amepanda kutoka nafasi ya tatu hadi ya kwanza kwa mujibu wa viwango vilivyotolewa na jana na mtandao wa mabondia Boxerec ambao hutoa viwango vya ubora wa mabaondia wale wa kulipwa na wasiowakulipwa. Katika viwango hivyo vinaonyesha mwakinyo pia ni wa 11 kwenye viwango vya ubora dunia kwa wanamasumbwi wa uzito huo wa kati. Bondia huyo mtanzania mwenye umri wa miaka 26 kutoka mkoani Tanga amepigana jumla ya mapambano 21ameshinda 19,13 kwa KO. Na amepoteza mapambano mawili tu.
1.Ni nafasi inayoshika timu ya Olimpiki ya Japan kwenye orodha ya timu zilizokusanya Medali nyingi za dhahabu sambamba na Marekani kwenye michezo ya Olimpiki inayoendela Tokyo Japan. Timu hizo zimeshachukua jumla medali 8 za dhabu, zikifuatiwa na China wenye medali 7 Urusi wana Medali 5 za dhahabu Uingerezawanashika nafasi ya 5 wakiwa na medali 4 za dhahabu.
Kwa ujumla Marekani na China ndio wanaoongoza kwa kuchukua medali nyingi wameshinda jumla ya Medali 19 wote kwa pamoja, wakifuatiwa na Urusi wenye medali 15, Japan wana medali 13 na timu ya Uingereza wameshinda medali 10.