Song asaini miaka minne na Spurs

Ijumaa , 23rd Jul , 2021

Nyota wa Tottenham Hotspur Son Heung-min asaini mkataba mpya wa miaka minne kuendelea kuitumikia Spurs na amedai ulikuwa ni uamuzi rahisi zaidi kwake, licha ya nyota mwenzake pacha Harry Kane kutaka kuvunja rekodi ya uhamisho wa pauni milioni 160 kwenda klabu ya Manchester City.

Heung-Min Son akishangilia moja ya bao aliloifungia Tottenham Hotspurs

Mkataba wa mshambuliaji huyo wa Korea sasa utaendelea hadi majira ya joto mwaka 2025, ambayo itamfanya awe amedumu klabuni hapo kwa miaka 10 baada ya kujiunga na klabu hiyo akitokea Bayer Leverkusen mwaka 2015.

Son mwenye umri wa miaka 29, amefunga magoli 107 na kutoa assist 64 katika mechi 280 alizocheza katika mashindano yote kwa kipindi cha misimu sita aliyoitumikia Tottenham hadi sasa.

Pia son ndio mchezaji aliyefunga goli la kwanza la Ligi Kuu na lile la Ligi ya Mabingwa kwenye uwanja mpya wa Tottenham Hotspur wanaoutumia hivi sasa.