Alhamisi , 8th Oct , 2020

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer hajawajumuisha Sergio Romeo, Phil Jones na Marcos Rojo, kwenye kikosi cha wachezaji 25 watakao cheza michezo ya klabu bingwa barani ulaya hatua ya makundi.

Sergio Romeo kulia alitaka kujiunga na Everton kabla ya dirisha la usajili kufungwa lakini usajili huo haukufanikiwa

Manchester United imepangwa kundi H pamoja na timu za Paris Saint-Germain, RB Leipzig na Istanbul Basaksehir, na mchezo wa kwanza watacheza dhidi ya PSG.

Mlinda mlango Sergio Romeo amejikuta nje ya kikosi baada ya kocha Ole Gunnar kuwapa kipaumbela zaidi magolikipa Lee Grant, Dean Henderson na David de Gea.

Msimu uliopita Romeo alikuwa golikipa namba mbili lakini baada ya Dean Henderson kurejea kutoka Sheffield United alipokuwa kwa mkopo msimu uliopita amejikuta nafasi yake ikiwa ndogo kwenye kikosi, na alihitaji kuondoka klabu hapo lakini inaaminika Manchester United ilizuia usajili wake wa kujiunga na klabu ya Everton.

Kwa upande wa mabeki wa kati Marcus Rojo na Phili Jones wao imekuwa ngumu kuingia kwenye kikosi cha kwanza kutoka na ushinda wa namba na kuzidiwa na wachezaji wengine wanaocheza katika nafasi hiyo kama Victor Lindelof, Eric Bailly, Harry Maguire, Timothy Fosu-Mensah na Axel Tuanzebe.

Wachezaji wote wapya waliosajiliwa msimu huu wamejumuhishwa kwenye kikosi hicho ambao ni Edinson Cavani, Alex Telles, Facundo na Donny van de Beek.

Kikosi kamili cha Manchester United cha wachezaji 25 kilichotajwa na kocha Ole Gunnar Solskjaer kitakacho cheza klabu bingwa ni

Makipa: David de Gea, Dean Henderson, Lee Grant

Mabeki: Eric Bailly, Timothy Fosu-Mensah, Victor Lindelof, Harry Maguire, Luke Shaw, Alex Telles, Axel Tuanzebe, Aaron Wan-Bissaka

Viungo: Bruno Fernandes, Fred, Daniel James, Jesse Lingard, Juan Mata, Nemanja Matic, Scott McTominay, Facundo Pellistri, Paul Pogba, Donny van de Beek

washambuliaji: Edinson Cavani, Odion Ighalo, Anthony Martial, Marcus Rashford