Ijumaa , 12th Dec , 2014

Timu za Simba na Yanga zinatarajia kukutana kesho Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam katika mechi ya Nani Mtani Jembe msimu wa Pili.

Akizungumza na East Africa Radio, Afisa Habari wa simba, Humphrey Nyasio amesema timu yake ipo vizuri katika maandalizi na wamejiandaa kwa ajili ya kushinda katika mechi hiyo hivyo mashabiki watarajie ushindi katika mechi hiyo.

Kwa upande wake, Mkurungenzi wa Masoko wa klabu ya Yanga, George Simba amesema watahakikisha wanalipiza kisasi cha mechi ya msimu wa kwanza ya mechi ya Nani Mtani Jembe ambapo walipata matokeo ya sare ya goli 3-3 suala ambalo hawakulitegemea.