
Simba kesho itakuwa dimbani kusaka taji lake la pili msimu huu baada ya kuchukua ubingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara. Itakipiga dhidi ya wenyeji wao Gor mahia ambao pia ni mabingwa watetezi.
Msemaji wa Simba Haji Manara, amesema wao kama Simba wana imani na uwezo wa kocha msaidizi Masoud Djuma ambaye kwasasa anaongoza timu hiyo baada ya kocha mkuu Pierre Lechantre kuondoka huku tetesi zikisema ametimuliwa.
Mbali na Masoud Djuma Manara pia amemtaja nahodha msaidizi Mohamed Hussein, ambaye kwasasa ni nahodha mkuu kutokana na John Bocco kutokuwepo kwenye kikosi kilichopo nchini Kenya, kuwa anajukumu la kuiongoza timu iweze kurudi na taji.
''Kocha Masoud Djuma wanasimba wana imani kubwa na wanajua una uwezo wa kuongoza kikosi kesho kwa kushinda na timu kucheza soka bora na Mohamed Hussein unajua thamani ya jezi ya Simba huku ukiwa na kitambaa cha unahodha, nendeni mkapigane kesho kwa faida ya nchi, klabu na maisha yenu'', ameandika Manara.