Ijumaa , 22nd Jul , 2022

RASMI leo Julai 22 Simba imemtambulisha beki mpya ambaye atakuwa kwenye kikosi chao kwa msimu wa 2022/23 katika mashidano ya kitaifa na kimataifa akichukua mikoba ya Pascal Wawa ambaye aliachwa rasmi na Simba.

Beki wa kati, Mohammed Ouattara kutoka Klabu ya Al Hilal ya Sudan.

Simba wenyewe wamemuita beki kisiki wa kuzuia mipira ya juu na chini, beki bora na mwenye uwezo wa kucheza kwenye kikosi chao anaitwa Mohamed Ouattara raia wa IvoryCoast.

Beki huyo aliwahi kufanya kazi na Kocha Mkuu wa Simba Zoran Maki kwenye Klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco na Al Hilal ya Sudan.

Ouattara ni mchezaji wa sita mpya kutambulishwa Simba msimu huu wa dirisha kubwa, wengine ni Moses Phiri, Habib Kyombo, Augustine Okrah, Victor Akpan na Nassor Kapama.

Simba kwa sasa imeweka kambi huko Ismailia, Misri kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.