Mechi ya Simba na Majimaji mzunguko wa kwanza, ambapo Simba ilishinda mabao 4-1
Mbali na mtanange huo utakaopigwa katika dimba la Majimaji Songea, Jijini Mbeya wenyeji wagonga nyundo wa jiji hilo wana koma kumwanya Mbeya City watawaalika masarange wa JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Sokoine
Ligi hiyo itaendelea tena siku Jumapili kwa mchezo mmoja baina ya matajili wa Mbagala wanalambalamba Azam FC wakipimana ubavu na wanakuchele timu ya Ndanda FC ya Mtwara kwenye Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi Mbande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam mchezo unaotarajiwa kuanza saa 1.00 usiku.
Na siku ya Jumatatu kutakuwa na mchezo mmoja tu ambako wana kishamapanda timu ya Toto Africans ya Mwanza itaikaribisha Ruvu Shooting ya Pwani kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Ligi hiyo itakwenda mapumziko wikiendi ya Februari 10, 11 na 12 kupisha michuano ya vilabu barani Afrika wakati wawakilishi wa Tanzania katika mchuano ya kimataifa Young Africans (Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika - CL) na Azam (Kombe la Shirikisho - CC) watakuwa na mechi za kimataifa.