Ijumaa , 9th Nov , 2018

Mabingwa wa soka wa Tanzania Simba SC, wamepangwa kucheza na timu ya Mbabane Swallows  ya Swaziland kwenye hatua za awali za ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2018/19.

Wachezaji wa Simba

Katika droo iliyofanyika leo, Novemba 9, 2018, jijini Cairo Misri yalipo makao makuu ya shirikisho la soka barani Afrika, Simba itaanza kampeni yake ya kimataifa kwa kukutana na wababe hao wa Swaziland katika hatua ya awali kabisa.

Simba itaanzia nyumbani mchezo ambao utapigwa kati ya Novemba 27/28 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam. Baadaye Simba itasafiri kuelekea Swaziland kwenye mchezo utakaopigwa kati ya Desemba 4/5.

Wawakilishi wa Tanzania Bara kwenye kombe la shirikisho Mtibwa Sugar watakuwa wenyeji wa Northern Dynamo ya visiwa vya Ushelisheli kabla ya kwenda ugenini kwaajili ya marejeano.

Wawakilishi wa Zanzibar kwenye ligi ya mabingwa Afrika ‪JKU wakakutana na Al Hilal ya Sudan aliyokuwa akiichezea Thomas Ulimwengu. Zimamoto ambao wanaiwakilisha Zanzibar kwenye kombe la shirikisho watakipiga na Kaizer Chiefs.