Jumatatu , 6th Feb , 2017

Timu ya Simba SC ya Dar es Salaam imepangwa kukutana na African Lyon katika mchezo wa raundi ya sita ya michuano ya Kombe la Shirikisho la TFF.

Kikosi cha Simba

Kwa mujibu wa matokeo ya droo yaliyotangazwa leo na Shirikisho hilo, mechi hiyo itachezwa katika dimba la Taifa Dar es Salaam tarehe 01, Machi mwaka huu.

African Lyon ndiyo timu iliyotibua rekodi ya Simba ya kutofungwa katika mechi zaidi ya 10 za ligi kuu Tanzania Bara msimu huu, na kuwa timu ya kwanza kuifunga Simba katika dimba la taifa Dar es Salaam kwa bao la dakika ya 90+3 lililowatia simanzi wapenzi na mashabiki wa Wekundu hao wa Msimbazi.

Wakati Simba wakipangwa kukipiga na African Lyon, watani zao Yanga wao watakutana na Kiluvya United ya daraja la Kwanza, ikiwa ni miongoni mwa timu mbili ambazo siyo za ligi kuu, zilizofanikiw kupenya katika raundi hiyo ya sita.

Mchezo wa Yanga na Kiluvya utakuwa  tarehe 7 Machi.

Ratiba kamili hii hapa....