Jumanne , 30th Dec , 2014

Klabu ya Simba ya jijini Dar es salaam imesema taarifa ya kumfukuza Kocha wa Timu Patrick Phiri hiyo sio za kweli kutokana na kamati ya utendaji kutotoa taarifa hizo.

Akizungumza na East Africa Radio, Afisa Habari wa Simba, Humphrey Nyasio amesema suala hilo litatolewa maamuzi pale suala hilo litakapotokea na mpaka sasa Phiri ni kocha wa timu hiyo.

Nyasio amesema, kamati ya utendaji na uongozi kwa ujumla ndiyo wenye mamlaka ya kutoa maamuzi na kama suala hilo lingekuwepo lingekuwa wazi.

Nyasio amesema, mpaka sasa bado kamati ya Utendaji ya Klabu hiyo inaendelea na mazungumzo na ikishamaliza mazungumzo hayo taarifa zitatolewa kwa wanachama na mashabiki wote kama mwalimu na ataendelea kuifundisha timu au ataondoka.

Pamoja na msemaji huyo kukanusha, taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinadai kuwa tayari kocha Patrick Phiri amekwisha kabidhiwa barua ya kutimuliwa kwake, na tayari kocha mpya anawasili kesho saa moja asubuhi.