Jumatatu , 7th Nov , 2016

Klabu ya Simba imesema, kufungwa na African Lyon katika mchezo uliochezwa hapo jana Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam hakuweza kuwakwamisha katika mbio zao za kuwania Ubingwa wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara.

Kikosi cha Prisons

 

Afisa habari wa Simba SC Haji Manara amesema, kufungwa ni sehemu ya mchezo na wao hawakupanga kutokufungwa katika michuano ya ligi bali lengo lao hasa ni kuchukua ubigwa na wanaamini bado nafasi ipo kwani bado mechi zipo nyingi.

Manara amesema, kikosi kimeondoka leo kuelekea Mbeya kuifuata Tanzania Prisons kwa ajili ya mchezo wake wa mzunguko wa nane ambao ulikuwa bado haujachezwa.

Simba ilipoteza mchezo wake dhidi ya African Lyon hapo jana mara baada ya kiungo wa African Lyon Abdallah Mguhi kuipatia timu yake bao pekee katika dakika za nyongeza za mchezo huo