Alhamisi , 19th Dec , 2019

Klabu ya Simba, leo Alhamisi, Disemba 19, 2019 imefungua ofisi mpya ya uendeshaji wa shughuli za kila siku za klabu hiyo Jijini Dar es Salaam maalum kama (Simba Corporate).

Ofisi mpya ya Simba SC

Ofisi hiyo inapatikana Diamond Plaza Ghorofa ya pili, Makutano ya Mtaa wa Mirambo na Samora Avenue.

Pia ofisi za awali zilizopo Mtaa wa Msimbazi Kariakoo, zitaendelea kutumika kwa shughuli na  mambo yote yanayahusu Wanachama na Mashabiki wa klabu hiyo, makumbusho ya klabu pamoja na duka.

Tazama hapa muonekano wa ofisi hiyo.