
Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ally
Hayo yamebainishwa leo na meneja habari na mawasiliano wa klabu ya Simba , Ahmed Ally alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari kuelekea maandalizi ya mwisho wa mchezo kuhitimisha kundi D na kusakata tiketi ya kuelekea hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
“kwenye mchezo wetu wa kesho mgeni rasmi atakuwa ni mheshimiwa Nape Nnauye ambaye ni waziri wa habari,mawasiliano na teknolojia ya habari na amekubali na kufurahia sanaa”amesema Ahmed Ally
Pia meneja huyo wa habari na mawasiliano wa klabu ya Simba amepiga marufuku mashabiki wenye mawazo ya kununua vitochi na kwenda kuwamulikia wachezaji wa timu pinzani kuacha mara moja kuhusu mpango huo kwani sio utamaduni wa klabu hiyo
"mliokuwa na mpango wa kununua vitochi au vitu vyenye mwanga achaneni navyo sisi makelele yetu ndio silaha yetu ya kushinda mchezo wa kesho" amesema Ahmed Ally