''Simba kama Simba lazima tuungurume sio kwasababu sisi ni wazuri sana ni kwasababu tumebaki na nafasi moja tu ambayo ni ligi hivyo lazima tujitoe tushinde ili tupate nafasi hiyo'', amesema.
Simba jana iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting hivyo kufikisha alama 38 kileleni mwa msimamo wa ligi. Simba inategemea ligi kuu pekee baada ya kuondolewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho na timu ya Green Worriors.
Kwa upande mwingine Masoud ameweka wazi kuwa kwasasa benchi lao la ufundi limekuja na mbinu mpya ambayo inaifanya timu ianzie kujilinda kwenye eneo la ushambuliaji ili kuzuia hatari kwenye eneo lake pamoja na kulazimisha timu pinzani ifanye makosa ili wayatumie kufunga.
Baada ya mchezo wa jana Simba itaingia dimbani tena Februari 7, siku ya jumatano kucheza na Azam FC inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo w aligi ikiwa na alama 33. Msimu uliopita Simba waliibuka mabingwa wa FA na kupata nafasi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

