Jumanne , 27th Mei , 2025

Kocha msaidizi wa Klabu ya Simba Suleiman Matola akizungumza kuelekea mchezo wao wa hapo kesho dhidi ya Singida Black Stars ameweka wazi umuhimu wa mchezo huo Akisisitiza ni lazima kushinda ili kujihakikishia ubingwa msimu huu.

Kocha msaidizi wa Klabu ya Simba Suleiman Matola

“Mechi ya Singida ni mrchi ya kiporo na haiwezi kuwa rahisi, Singida ni moja ya timu ngumu sana, timu ambayo imewekeza, ina wachezaji wazuri, timu ambayo katika ligi inasumbua ila sisi kama Simba tumejipanga, pamoja na ugumu wao Singida lazima tupate matokeo ya alama tatu kesho.

Ratiba imekuwa ngumu, nafikiri duniani kote hakuna kocha ambaye anapenda kucheza kila baada ya siku mbili lakini tulilijua mapema namna gani ya kukabiliana nayo''

''Suala la rotation lipo chini yetu waalimu, kwahiyo tutaangalia baada ya mazoezi ya leo, kikubwa ni kwamba timu nzima ipo kambini na wachezaji wote wapo vizuri, ni sula la benchi la ufundi kuona nani aanze na nani asianze.

Kila mchezo una plan yake, fainali ishaisha licha ya suala la saikolojia baada ya kupoteza mchezo wa fainali halikuwa sawa ila wachezaji wetu ni wakomavu baada ya fainali tulisema kwamba hili limekwisha, targate yetu sasa ni kuhakikisha tunapta kikombe Ligi kuu na hatuwezi kuwa mabingwa kama hatutoshinda mchezo wa kesho” -Seleman Matola Kocha Msaidizi Simba SC