Ijumaa , 17th Oct , 2014

Mechi za Msimu wa kwanza mzunguko wa Nne wa Ligi kuu Tanzania Bara zinaendelea kesho nchini kwa mechi Sita kupigwa katika viwanja mbalimbali nchini huku mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga ikipigwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

Wachezaji wa Simba na Yanga wakisalimiana

Akizungumza jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Boniface Wambura amesema katika mechi hiyo Jeshi la polisi limejipanga kwa ajili ya mashabiki wanaofika uwanjani kwa ajili ya Vurugu.

Wambura amesema tiketi kwa ajili ya mechi hiyo hazitauzwa uwanjani hapo kwa kesho hivyo mashabiki wakate tiketi mapema kabla ya kufika Uwanjani.