Ijumaa , 14th Oct , 2016

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea kesho Jumamosi Oktoba 15, 2016 kwa michezo mitatu kupigwa katika viwanja tofauti.

Baadhi ya wachezaji wa Simba SC katika dimba la Uhuru DSM

Simba inayoongoza katika msimamo wa kuwania taji hilo katika timu 16 itaikaribisha Kagera Sugar ya Kagera kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mchezo mwingine utakuwa ni kati ya JKT Ruvu na Mwadui ya Shinyanga utakaofayika Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani ambako.

Pia Stand United ya Shinyanya itaikaribisha African Lyon kwenye Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga.

Ligi hiyo itaendelea keshokutwa Jumapili kwa mchezo utakaozikutanisha timu za Azam na Young Africans zote za Dar es Salaam mchezo utakaopigwa katika dimba la Uhru Dar es Salaam na kuchezeshwa na mwamuzi Israel Ngongo.

Michezo mingine siku hiyo itakuwa ni: Ruvu Shooting na Mbeya City kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani, Mtibwa Sugar ya Morogoro na Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro na Toto African itakayokuwa mwenyeji wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.