Hii itakuwa mara ya pili kwa Timu hizi kukutana kwenye Mashindano haya kwani walikuwa Kundi moja ambapo katika mchezo wa makundi Mtibwa Sugar iliifunga Simba 1-0.
Mchezo huu una umuhimu kwa pande zote Simba wakihitaji kulipa kisasi cha kuchapwa katika mchezo wa kwanza na kumpa kikombe cha kwanza kocha wao mpya Goran Kopunovic.
Kwa upande wa Mtibwa wanahitaji kushinda mchezo huo ili kuendeleza ubabe wao kwa kuwafunga Simba na kutwaa ubigwa wa kombe la Mapinduzi .
Michuano hii maalumu kwa ajili ya kumbukumbu za mapinduzi ya Zanzibar ilianza Januari Mosi kwa kushirikisha jumla ya timu 12.