
Barbara Gonzalez
“Kikosi chetu ni kizuri na tukipewa malengo makubwa tutayafikia na kule Angola kila wakisikia jina la Simba, Simba walikuwa na hofu na kila nchi Watu wanahofu na Simba, hata Viongozi tuliokuwa nao kule jukwaani wa De Agosto walikuwa na hofu na najua watakuja hapa wakiwa na hofu dhidi ya Simba”amesema Barbara Gonzalez
Simba imerejea leo kutokea Luanda nchini Angola baada ya kupata ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Premiero De Agosto kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika huku wakitaraji kurejeana Jumapili ya Oktoba 16, 2022 kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam