Ijumaa , 30th Jan , 2015

Michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea kesho kwa kuzikutanisha Simba SC ikishuka dimbani kupambana na JKT Ruvu uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam huku Coastal Union yenyewe ikiikaribisha Mtibwa Sugar uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Mechi nyingine zitakazopigwa kesho ni Ruvu Shooting itakayoikaribisha Stand United uwanja wa Mabatini, Kibaha Mkoani Pwani ambapo Kagera Sugar itakuwa mgeni wa Tanzania Prisons na Polisi Morogoro itaikaribisha Mbeya City uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Mzunguko huo utamalizika kwa kuzikutanisha Yanga na Ndanda FC zitakazoshuka uwanja wa Taifa jijini
Dar es salaam.